Social Icons

FLORA BIDHAA 3

FLORA BIDHAA 3

FRORA BIDHAA 4

FRORA BIDHAA 4

FLORA MBASHA BIDHAA 1

FLORA MBASHA BIDHAA 1

FLORA BIDHAA2

FLORA BIDHAA2

Monday, February 9, 2015

HABARI ZA MITANADAONI (RUMAFRICA) KUHUSU FLORA MBASHA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

Flora Mbasha ambaye amejifungua mtoto wa kike hivi karibuni, amemshukuru Mungu kwa kujifungua na kwa kumpigania tangia alivyokuwa mjamzito. Akiongea na Rumafrica amesema, kwa sasa anaendelea vizuri sana na Mungu anazidi kumpigania na kumlinda yeye na familia yake.

Flora Mbasha

Pia amewashukuru madaktari waliokuwa bega kwa bega katika kipindi chake cha ujauzito mpaka alipojifungua na bila kuwasahau ndugu zake na marafiki zake ambao walitumia muda wao kumuombea na wengine kumsaidia kwa njia mbalimbali.

Akiongea kwa msisitizo aliwashukuru sana ndugu zake anaoishi nao nyumbani kwake kwa kipindi chote alichokuwa nao, wamevumilia mengi na wamekuwa msaada mkubwa sana katika maisha yake. Na hasa alimshukuru sana mama yake ambaye amekuwa mtu wa kwanza kumfariji kipindi cha ujauzito wake na jinsi alivyokuwa akitumia muda wake kuja kumtembelea.

Flora Mbasha ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, amezidi kuwashukuru wadau wake wanaonunua kazi zake (DVD), kwa kufanya hivyo wamekuwa msaada mkubwa sana kwake kujipatia kipato na pia kutimiza ndoto yake ya kusambaza Neno la Mungu kwa kupitia uimbaji. Pia amewashukuru wachungaji na waimbaji wa nyimbo za injili ambao wamekuwa wakimualika katika matamasha na mikutano mbalimbali...Anaamini kuwa kuna watu wengi wamebarikia kitabia na kimaisha kwa kupitia huduma yake hii ya uimbaji.

Flora Mbasha ambaye kwa sasa ni mjasiriamali mkubwa amewataka wadau wakumbuke kuwa yeye anajihusisha na uuzaji wa vitu mbalimbali kama vile viatu, vikapu, mabegi, nguo, urembo n.k, kwahiyo amewaomba watu wote kuweza kununua bidhaa zake.

Rumafrica iliweza kumdodosa kuhusu huduma yake ya uimbaji, naye alisema, sasa naingia kwa miguu yote miwili katika kumtumikia Mungu wangu kwani nimekuwa kimia sana kiuimbaji kwa muda mrefu kutokana na hali yangu ya ujauzito, lakini sasa Mungu amenisaidia niko vizuri sana kihuduma, watu wategemeee kupata vitu vipya ambavyo Mungu ameweka ndani yake kwa kipindi kirefu.

Unaweza kutembelea www.florambasha.blogspot.com kujua mengi kuhusu Flora Mbasha na pia kupata mawasiliano yake.

MUNGU AWABARIKI SANA

No comments:

Post a Comment